JINSI YA KUFANYA MANUNUZI KWENYE MTANDAO WA ALIBABA NA ALIEXPRESS - MotechBoy

MUBASHARA

Sunday, August 11, 2019

JINSI YA KUFANYA MANUNUZI KWENYE MTANDAO WA ALIBABA NA ALIEXPRESS


Karibu Mpenzi msomaji wa blog ya MotechBoy,leo nawaletea utaratibu wa kuagiza bidhaa mtandaoni kupitia Alibaba na Aliexpress.

Kwanza kabisa elewa kuwa hizi ni online markets chini ya mwamvuli mmoja au kwa maana nyingine ni mitandao chini ya umiliki mmoja. Alibaba ndio mtandao mama uliouzaa aliexpress, tofauti yake ni kwamba, alibaba ni B2B na aliexpress ni C2C marketplace. Inawezekana hujui nini maana ya B2B na C2C nitawaeleza wakati mwingine.
1.     Alibaba.com
Alibaba ndio soko kubwa kuliko yote kwenye mtandao. Hapa utapata karibu kila aina ya bidhaa unayoitaka kutoka kwa wauzaji pande zote za dunia japo kwa wachina ndio zaidi. China inakua katika maendekeo ya viwanda kwa kasi kubwa sana, kuna viwanda na makampuni toka nchi zingine ikiwemo Marekani wanatengenezea bidhaa zao China mfano kampuni ya Apple nchini Marekani inatengenezea bidhaa China na zimeandikwa “made in China” huo ni mfano mmoja kati ya mingine mingi. Sababu kubwa ni kuwa wanatumia “cheap labour” yani malipo ya wafanyakazi sio makubwa kama Marekani. 
Jinsi ya kununua
  • Kwanza fungua akaunti yako kwenye mtandao wa alibaba ambapo hamna malipo ya kufanya hivyo. Pale utakutana na sehemu za kujaza mfano jina lako, email address, anwani yako, jina la kampuni (kumbuka hii ni B2B ndio maana utatakiwa kujaza kampuni) usiogope kama huna kampuni wewe jaza tu sifa ulizonazo. Hata mimi kabla sijawa na kampuni nilijaza kama mtu binafsi.
  • Baada ya kufungua akaunti alibaba sasa upo tayari kuweza kufanya manunuzi. Unapohitaji kununua, ingia hapa halafu tafuta unachohitaji kwa kutumia search engine yao kwenye ukurasa wa nyumbani (home page). Utaletewa bidhaa ya aina hiyo kutoka kwa makampuni lukuki yanayouza na kwa bei tofauti tofauti pamoja na viwango vya uwingi au ubora tofauti. Utachagua bidhaa na muuzaji ulieridhika naye.
  • Ukishachagua bidhaa utatuma “buying request” kwa muuzaji na utajaza form maalumu ambayo imetengenezwa pale, wewe ni kubonyeza tu halafu itakuongoza. Baadaye muuzaji akikujibu, mtaanzia hapo mazungumzo yenu hadi mtakapokubaliana bei na mambo kama hayo.
  • Mkishakubaliana, muuzaji atatengeneza mkataba kati yako na yeye ambao hadi naandika maelezo haya huo mkataba una kichwa kisemacho “SALES AND PURCHASE ORDER”. Huo mkataba ni wakati wako kuusoma kwa makini ili uone ulivyoandikwa kama ndivyo mlivyokubaliana na muuzaji. Mambo muhimu kuangalia katika mkataba huo ni kama yafuatayo; jina na aina ya bidhaa, idadi pamoja na delivery terms ni CNF au CIF?.
  • Ukisharidhika na huo mkataba basi utaupokea na kama unamapungufu basi utamwambia muuzaji aurekebishe. Kwa hiyo ni muhimu sana usome mkataba na kama labda huelewi vizuri lugha ya kiingereza unaweza kuomba msaada wa ufafanuzi kwa rafiki au ndugu.Basi utakapoona kuwa mkataba upo sahihi basi ukubali na hatua zingine zifuate.
  • Baada ya kukubaliana na mkataba, wewe utatakiwa kulipa pesa kwa njia ya Safe Trade,ambayo  ni ''Safe Transanction'' au malipo salama  
  • Baada ya kulipa pesa, muuzaji atatakiwa ndani ya siku kumi na tano (15) atume mzigo wako. Baada ya kuutuma, atatakiwa aonyeshe hati za kutumia huo mzigo (Shipping Documents) kupitia mtandao wa alibaba. Mara nyingi ataonyesha kuwa wewe utapokea nakala za hizo hati maana kama atatuma hati original itamchukua     mda mrefu hadi apewe hela yake. Usiogope ukisikia kuwa utapata nakala tena uta “download” wewe mwenyewe kwenye mtandao maana najua unajua kuwa     bandarini hawapokei nakala kivuli bali nakala halisi. Ukweli ni kuwa bandarini hupokea nakala kivuli za hati (Bill of Lading) ila inatakiwa kampuni ilyosafirisha huo mzigo iwe imetoa hati maalumu inayoitwa TELEX RELEASE, kwa hiyo ukiwa na nakala iliyoandikwa hivyo pale bandarini (Shipping Line) wataithibitisha na hautapata shida.
  • Muuzaji akishatuma mzigo na akaonyesha hizo document kwenye mtandao, basi wewe utatakiwa kuthibitisha “confirm” malipo ili apewe muuzaji. Kama hautafanya hivyo, mfumo wa alibaba utalipa automatically ndani ya siku kumi (10) upende usipende.
Hongera, baada ya kupitia hatua hizo sasa kaa chini usubiri mzigo wako utakaokuja na meli au ndege na utafika kwa muda usiopungua siku mbili mpaka tatu hii ni kwa ndege na kwa meli ni kuanzia wiki mpaka mwezi.

Jinsi ya kufanya manunuzi kwenye mtandao wa Aliexpress
2. Aliexpress.com
Aliexpress ni mtandao pacha wa alibaba. Wakati alibaba ni B2B hii aliexpress ni C2C.
Kama nilivyosema kuwa aliexpress ni mtandao pacha wa alibaba, hapa huna haja ya kufungua akaunti nyingine na utatumia ile ile ya alibaba (anuani ya barua pepe kama user name na neno la siri lile lile). Hatua gani sasa za kuzipitia  kuelekea ukamilifu wa manunuzi yako ni kama ninavyoeleza hapa chini.
  • Hapa pia utaangalia bidhaa unayotafuta kupitia search engine yao iliyo juu kabisa kwenye ukurasa wao wa nyumbani. Baada ya kupata bidhaa unayopenda na ukaridhika nayo utaiweka kwenye kikapu “add to cat” kabla ya kuinunua. Kwa bahati nzuri aliexpress ina mfumo wa haraka wa kupiga hesabu zote hadi ulipo, kwa hiyo wakati mwingine huna haja ya kuwasiliana na muuzaji kwani kila kitu utakipata pale kwa mfano mzigo ukitumwa kwa DHL au FEDEX ni bei gani na ukitumwa kwa SingaporePost au HongKong Post ni shilingi ngapi.
·   Mpaka hapa najua kuwa bidhaa yako tayari ipo kwenye kikapu “cat”, basi bonyeza kikapu na idadi ya bidhaa zako ulizoziweka kwenye kikapu zitasomeka zote. Chagua     unayotaka kuilipia au unazotaka kuzilipia kama ni zaidi ya moja. Kisha tafuta mahali palipoandikwa “place order”, ukishapaona bonyeza hapo na utaletwa kwenye         
   sehemu unayotakiwa kujaza tarifa zako za kadi ya benki na utazijaza pale kama inavyohitajika.
  • Baada ya kujaza details zote za kadi yako sasa utabonyeza “pay my order”, kisha utapokea ujumbe kwenye kioo cha komputa yako ukisema malipo yako yamepokelewa na aliexpress na sio muuzaji. Na yatahakikiwa ndani ya masaa 24 kabla muuzaji hajatumiwa taarifa kuwa umelipa na anatakiwa afanye mchakato wa kutuma mzigo.
  • Kwa kawaida hiyo bidhaa utakuwa umeshafahamu itatumwa baada ya muda gani maana ni lazima paandikwe muda mwafaka utakaotumika kuchakata oda yako “processing time”. Basi ndani ya huo mda mzigo utatumwa na utapata ujumbe kupitia anuani yako ya barua pepe. Utaingia kwenye akaunti yako ya aliexpress na utakuta tracking number ya huo mzigo.
  • Utasubiri mzigo wako hadi ufike, uridhike nao ndio muuzaji alipwe pesa. Hapa ni tofauti na malipo ya ule mzigo unakuja kwa bandari ambapo muuzaji atalipwa baada tu ya kuonyesha documents za kutumia mzigo.
Mzigo ukishakufikia, utauangalia kama ndio wenyewe au vinginevyo, kuna uwezekano mkubwa sana wa kutumiwa mzigo tofauti.
Kama utakuta tofauti na ulivyonunua, basi utafungua kesi kudai aidha urudishiwe pesa yako au utumiwe mzigo mwingine. Namna ya kufungua kesi imeelezwa wazi kwenye oda hiyo ambayo hadi muda huo inakuwa haijafungwa.

Asante kwa kusoma makala hii ukipata shida yoyote usisite kunitaarifu.

14 comments:

  1. Nimeipenda makala yako mkuu.natamani san nifanye hii kitu.... Nakupata je kwa msaada zaid

    ReplyDelete
  2. Naomba ushauri ni suppliers gani, wako trusted alibaba kwenye mambo ya laptops

    ReplyDelete
  3. Samahani naomba kujua, je nitajuaje kama mzigo umeshafika?

    ReplyDelete
  4. Umeeleza vizuri lkn hujafafanua kwa upande aliexpres wanatumia njia gani mpaka kukufikia mzigo mkononi je wana wakala au je au utalipa ushuru tra maana sisi wengine tunaeeza kimbilia kununua kumbe ikifika dar kukawa kuna mambo mengi mwisho ukasemehe mzigo

    ReplyDelete
  5. Vipi kuhusu tozo za bandari je gharama hizo utakazo lipia zinahusu gharama za usafir na tozo za bandarini

    ReplyDelete
  6. Nimekubal msahada wako
    Naomba kuuliza alibaba wapo kama kikuu(mzigo unaupokelea ofisin kwao) au mzigo unaupokea bandarini

    ReplyDelete
  7. Asante sana.. Kwani kuna tozo hani zaidi mzigo ukifika bandarini? Na pia unafikaje mikoani?

    ReplyDelete
  8. Kwa huduma za kutuma mizigo Kwa ndege kutoka China
    Wasliana nasi
    0656676717
    Instagram @ smart_express

    ReplyDelete
  9. Nimeioenda Sana Sana makala yako vipi nakupataje

    ReplyDelete

Pages