Watu sikuizi wanapenda vitu vizuri na ukiangalia kadri dunia inavyobadilika na watu pia hubadilika hasa kwenye upande wa magari hahuna asiyependa kuendesha gari sivyo🙄
kuna njia nyingi za kuiboresha gari yako mwenyewe, kwa gharama nafuu zifuatazo NI sehemu kuu ambazo unaweza kulifanya gari lako kuwa Bora zaidi.
1. Ongeza spika
Ukiongeza spika katika gari lako litakufanya kuburudika zaidi pindi uwekapo mziki mzuri na kukufanya kuwa na furaha wakati wote uendeshapo gari.
2. Badilisha Rangi
Kusema ukweli gari ni rangi pasipo rangi hakuna gari kwani gari ndo linakupa muonekano kamili was gari lako,pindi uchaguapo rangi nzuri ndivyo gari lako litazidi kuvutia
3. Badilisha Rims Zako au Zipake Rangi
Moja kati ya sehemu nzuri katika gari yako ni rims Kama gari lako Lina rims nzuri litakuwa lakuvutia Sana haswa ukichagua rims ambazo ziko kwenye soko la magari ama trends kuna hizi alloy rims/wheels ni nzuri Sana kama ukiziweka kwenye gari lako.
4. Badilisha kasha ya Steering Wheel
Naam,ukiongelea gari hapa ndipo kwenye mkazo jitahidi Sana kuboresha gari lako hili eneo maana watu wengi hupasahau hapa wakati ndipo penye matumizi ya Kila siku ukiwa na cover nzuri za steering Mambo yenakuwa Bomba kabisa.
5. Badilisha Kichwa cha Gia
Ukibadilisha kasha la steering, badilisha na kichwa cha gia ili kusudi vifanane ili kupata mvuto mzuri wa gari lako.
6.Weka Tint
Ukiweka tint kwenye gari lako utakuta umeliongezea muonekano mwingine mzuri.
7. Taa za Nje
Utaweza kuona vizuri zaidi kwa kuongeza taa za nje. Pia, utalifanya gari lako kuwa na muonekano mzuri
8. Mfumo wa Usalama
Hakikisha gari lako lina mfumo wa usalama yani alarm ili kukuongezea ulinzi wa gari lako
9. Weka tv
Weka tv ili uweze kupata Raha kamili ya gari yako kwani tv husaidia kupamba gari lako na kulifanya la kisasa zaidi
10. Namba za Usajili za kipekee/plate namba
Hapa waweza kuweka namba zako mwenyewe binafsi au kuweka jina lako ila itakubidi ufuate utaratibu wa kubadirisha plate namba zako.
No comments:
Post a Comment