JINSI YA KUFUNGUA PATTERN AU PASSWORD YA SIMU YOYOTE - MotechBoy

MUBASHARA

Tuesday, October 1, 2019

JINSI YA KUFUNGUA PATTERN AU PASSWORD YA SIMU YOYOTE



Umesahau Password / Pattern lock ya simu yako? 
Kuna njia mbalimbali za kutoa lock ya pattern kama umeisahau katika Smartphone yako ya Android.
Njia hizo ni:-
1 Hard reset na
2. Password/security /pattern files kwenye Linux Operating System 

Leo hii tutajifunza jinsi ya ku-Unlock pattern kwenye simu kwa kutumia njia ya kwanza tajwa hapo juu.

Hard Reset

Hii ni moja ya njia rahisi kabisa ambayo kila mmoja wetu anaweza kuitumia katika simu yake ya Android endapo itatokea umesahau pattern au Password.

Onyo!: 
Njia ya Hard Reset ina tabia ya kufuta data zilizohifadhiwa kwenye simu.
Data hizo kama
1. Majina ( contacts ) yaliyohifadhiwa kwenye phone's memory

2. Videos na picha zilizopo kwenye memory ya simu

3. Applications zilizodownloadiwa kwenye simu yako
( Apps za default hazitafutika)

Step za kufuata ili kutoa Lock ya pattern kwenye Android Smartphone 

1. Hakikisha Chaji ya simu yako ipo angalau asilimia 50 na kuendelea

2. Izime simu yako kisha toa Memory Card pamoja na Sim card

3. Iwashe simu kwa kubonyeza kitufe cha kuongeza sauti pamoja na cha kuwashia simu kwa pamoja na vishikilie mpaka simu itakapowaka kwa kukupeleka kwenye recovery mode

Hatua hii hukataa kwa baadhi ya simu. kama simu yako ni moja kati ya simu hizo basi jaribu kutumia combination zifuatazo hadi itakapo kubali,
a. Volume up + home +power
b. Volume down +power
c. Volume up + power
d. Volume down +home +power
e. Home +power



Volume up ==>> Ni kitufe cha kuongeza sauti
Volume down==>>Ni kitufe cha kupunguza sauti
Power==>>Ni kitufe cha kuwasha simu
Home==>> Ni kitufe cha Nyumbani 
( chenye alama mithili ya nyumba au O na hukaa katikati ya simu)


 Baada ya simu kuwaka na kuleta Recovery mode, itakuletea muonekano wa picha hii hapa chini.
factory-reset-kwenye-android
Kuna baadhi ya simu huleta maandishi ya kichina na kuleta muonekano wa dizain hii
pattern-simu-inaleta-maneno-ya-kichina
4.  Tumia button za sauti kwa kupandisha au kushusha na kuchagua wipe data/factory reset ( au mstari wa tatu kutoka chini kwa simu zenye maandishi ya kichina kama inavyoonekana kwenye picha ya hapo juu ) kisha bonyeza kitufe cha kuwashia simu kuashiria OK.

5. Simu itaanza ku-reset yenyewe na baada ya kumaliza italeta muonekano kama huu wa kwenye picha ya hapa chini
pattern-unlock-kwenye-simu
6. Baada ya hapo chagua Option yarestart. 
Simu yako itwaka na haiitaka kukuficha kitu chochote kile kwa kukudai Password au Pattern. 

No comments:

Post a Comment

Pages