FAHAMU KUHUSU ECOMMERCE - MotechBoy

MUBASHARA

Tuesday, August 27, 2019

FAHAMU KUHUSU ECOMMERCE

Tokeo la picha la ecommerce hd images


Je, ulikuwa ukijiuliza maswali mengi kuwa unaanzaje kuuza au kununua kwenye intaneti? Hapa utajifunza nini maana ya eCommerce na namna inavyofanya kazi,karibu.
Maana ya eCmommerce ni kitendo cha kuuza au kununua bidhaa na/au huduma kwa njia ya intaneti.
Makundi makuu ya eCommerce
B2B (Business to Business)
Ni mfumo wa biashara unaohusisha wenye viwanda wakiwauzia wafanya biashara wakubwa wanaouza kwa jumla au kiwanda kwa kiwanda wakiuziana au mfanya biashara wa jumla akimuuzia mfanya biashara mwingine auzaye kwa jumla. Mfano wa masoko hayo ya B2B ni kama alibaba.com, made-in-china.com, globalsources.com, tradett.com na mengine mengi.
Habari njema ni kwamba hata wewe mnunuaji wa kawaida kama unataka kununua bidhaa moja kutoka B2B inawezekana hasa kwa alibaba.com. Cha kufanya wakati unataka kununua nwambie muuzaji kuwa unanunua sampuli (commercial sample), hapo unaweza kununua hata memory card moja ya Mb128 na watakutumia. Nisemapo memory card ya mb128 sitanii, mimi mwenyewe nimewahi kununua hivyo. Moja ya sababu za maendeleo waliyoyapata wachina ni pamoja na uwezo wao wa kuuza bidhaa kuanzia moja kwa bei yoyote na wako tayari kukuhudumia sawa na anayenunua bidhaa za kujaa kontena la futi 40.
C2C (Consumer to Consumer)
Huu ni mfumo wa kibiashara ya intaneti ambao unahusisha mtu na mtu wakiuziana bidhaa moja au zaidi. Hapa unaweza kuuza au kununua bidhaa ya aina yoyote hata kama ni ndogo na kwa thamani ndogo. Mfano wa masoko haya ni kama aliexpress.com, ebay.com, craiglist.com, etsy.com na mengine mengi.
B2C (Business to Consumer)
Kundi hili linahusisha wauzaji wakubwa au viwanda kuwauzia makundi ya wateja aina zote. Hapa pia hutumika mifumo ambayo hakuna mtu katikati wa kuweza kumwuliza (hadi ikibidi) kwani kila kitu unakuta kimewekwa bayana na hiyo mifumo kwa maana ya muundo wa hiyo bidhaa (specifications/descriptions), bei hadi ulipo (CIF), mzigo unatumwaje na shirika gani na unaweza kuchagua shirika gani ulitumie kusafirisha na bei zake, kwa hiyo unakuta kila kitu kimewekwa na hiyo mifumo hivyo huna haja ya kuuliza mtu. Mfano amazon.com, ebay.com, aliexpress.com na masoko mengine.
C2B (Consumer to Business)
Hapa unakuta mtu binafsi (end user/consumer) anaweka bidhaa yake au huduma kwa njia ya mnada, kisha makampuni yanashindana dau. Baadae huyu muuzaji binafsi anachagua kampuni gani aiuzie hiyo bidhaa au huduma. Mfano wake ni kama elance.com na mengine. Hata hii tovuti unayoendelea kusoma ni moja ya wadau wa C2B kupitia Google AdWords na AdSense. Ukiangalia juu na pembeni mwa kurasa nyingi za tovuti utaona matangazo ya makampuni mbalimbali ambayo yanalipia hayo matangazo. Kwa maana rahisi tunawauzia huduma ya kutangaza biashara zao. Kwa hiyo mfano mimi ninayetoa mada hizi ni mtu binafsi na ninatoa huduma kwa makampuni makubwa, viwanda nk. Hapo nakamilisha maana ya C2B kwamba mtu (end user/consumer) anauza bidhaa au huduma kwa makampuni.

No comments:

Post a Comment

Pages