FAHAMU KUHUSU INCOTERMS,CIF,CNF.FOD - MotechBoy

MUBASHARA

Tuesday, August 27, 2019

FAHAMU KUHUSU INCOTERMS,CIF,CNF.FOD










       






Tokeo la picha la cif,cnf hd images










INCOTERMS (International Commercial Terms) ni maneno ya kawaida sana katika biashara yoyote ya kimataifa bila kujali ni njia gani inatumika aidha kwa intaneti au ana kwa ana. Hautaweza kuuza au kununua bidhaa nje ya nchi bila kukutana na maneno haya. Hizi incoterms zipo chini ya sheria ya biashara ya kimataifa ambazo huratibiwa na bodi ya International Chamber of Commerce (ICC) yenye makao yake makuu Paris nchini Ufaransa.
Maneno haya hayajaanza kutumika sambamba na teknolojia hii mpya ya biashara kwa njia ya intaneti, la hasha! Incoterms zina umri mkubwa zaidi tangu mwaka 1936, zimekuwa zikirekebishwa kulingana na mabadiliko na mahitaji ya wadau. Hadi sasa zimeshabadilishwa mara sita na toleo linalotumika kwa sasa ni la 2010 na linatumika kwa kila nchi duniani inayohusika na kuuza au kununua kutoka nchi nyingine kupitia intaneti au ana kwa ana.
Wengi hawajui maana ya maneno haya hasa wanaoanza kununua au kuuza kwa njia ya mtandao wa intaneti. Na wengine tayari wapo kwenye utata baada ya kununua bidhaa ambayo iliuzwa kwa mfumo wa CNF. Kupitia mada hii na utafahamu maana ya hizi INCOTERMS na jinsi zinavyotumika. Ni muhimu kabisa kuifahamu kabla hujaanza kununua ili kukwepa utata unaoweza kukukumba. Katika aya zinazofuata zimetajwa na kuelezewa moja baada ya nyingine hasa ambazo zinatumika mara nyingi maana kuna zingine chache hazitumiki mara kwa mara.
EXW (Ex-works)
Hapa inamaanisha kwamba bei ni ya kiwandani tu! Garama za kutoa mzigo kiwandani zinamuhusu mnunuzi pamoja na garama zingine zote zitakazofuata. Mfano bidhaa inauzwa labda China kwa USD 2400 EXW na wewe umekubali kuinunua ukiwa Tanzania, ina maana kwamba hiyo bidhaa ipo kiwandani, wewe utaenda kuichukua kiwandani na namna gani unaisafirisha hadi bandarini au uwanja wa ndege utapanga wewe, na garama zingine kama ushuru na kila kitu hadi mzigo ufike Dar es Salaam ni wewe mwenyewe unahusika. Muuzaji hahusiki na chochote zaidi ya kukukabidhi mzigo wako na kukupa risiti pale kiwandani kwake. Hivyo ndivyo ilivyo kwa upande wa EXW ambayo ni kifupi cha Ex-works na wakati mwingine huandikwa Ex-factory.
FOB (Free on Board)
Hapa ni kwamba muuzaji ametoa bei inayohusisha kuinunua bidhaa na yeye atahusika kuisafirisha hadi bandarini au uwanja wa ndege tu! Garama zingine baada ya hapo utajua wewe mwenyewe mnunuaji. Mfano bidhaa inauzwa China kwa USD 3700 FOB, ina maana kuwa hiyo bei inahusu garama za kununua na kufikisha mzigo bandarini au uwanja wa ndege. Baada ya hapo wewe (mnunuaji) utahusika na kila garama nyingine hadi ufikishe mzigo waka Dar es Salaam. Hivyo ndivyo FOB (Free on Board) ilivyo, wakati mwingine huitwa Freight on Board.
CNF (Cost and Freight)
Hapa muuzaji anapotaja bei ujue atahusika kukuuzia, kuisafirisha hadi bandarini au uwanja wa ndege, kuhusika na ushuru (customs clearince) kwa upande wa nchi yake na pia kuisafirisha hadi bandari yako ya karibu utakapomwambia. Mfano muuzaji amekuandikia bei USD 2900 CNF Dar es Salaam. Hapo fahamu kuwa mzigo utasafiri toka huko mbali na shuruba za njiani wakati hauna bima (nadhani unajua umuhimu wa bima). Wewe utahusika na garama zingine mfano hiyo bima, ukaguzi pamoja na garama zote za ushuru kwa upande wa Tanzania. Hivyo ndivyo ilivyo CNF (Cost and Freght), wakati mwingine huitwa Cost No insurance, Freight au CFR
CIF (Cost, Insurance, Freight)
Kwa upande wa CIF, muuzaji atajapo bei basi yeye atahusika na garama zote ikiwemo bima hadi kufikisha mzigo wako kwenye bandari au nchi yako. Mfano muuzaji nchini China ameandika bei ya bidhaa labda USD 5000 CIF Dar es Salaam. Basi tambua kuwa muuzaji atahusika na garama zote hadi bandari ya Dar es Salaam na wewe utahusika na garama kuanzia bandari ya Dar es Salaam kwa maana ya ushuru na garama zingine hadi kuufikisha mzigo unakoupeleka mwenyewe.
DAP (Delivered At Place)
Hii ni Incoterm nyingine ambayo inahusu muuzaji kuuza na kukuletea bidhaa hadi mlangoni kwako. Mnunuaji unaponunua bidhaa utasubiri nyumbani au kwenye duka au ghala (ware house) lako ila utahusika tu na mambo ya forodha kwa upande wa Tanzania. Mfano muuzaji ameandika labda USD 8,000 DAP, Tanzania, Mwanza - Pamba Avenue. Hapo wewe mnunuaji uliyepo Mwanza utalipa pesa na kusubiri uletewe mzigo wako hadi mtaa wa Pamba Mwanza. Muuzaji atagaramia usafiri toka China hadi Dar es Salaam, wewe utalipia ushuru na garama zingine zitakazohusiana halafu kutoka hapo muuzaji atatumia kampuni ya usafirishaji (Clearing and forwarder) kuweza kukuletea mzigo Mwanza na atakuwa amelipa garama zote za usafiri.
DDP (Delivery Duty Paid)
Hapa muuzaji akiandika bei ufahamu kwamba ukilipa basi kunja mikono kabisa kwani hautakunjua kqa malipo yoyote. Mfano muuzaji nchini China anauza bidhaa na akaandika USD 20,000 DDP, Tanzania, Mwanza - Pamba Avenue basi fahamu kuwa wewe ukilipa hiyo pesa hauyahusika na garama nyingine yoyote. Utasubiri mzigo wako tu. Hivyo ndivyo ilivyo DDP (Delivery Duty Paid) au wakati mwingine huitwa Door delivery Duty Paid.
C&I (Cost and Insurance)
Hapa ni kwamba muuzaji atahusika kukuuzia bidhaa na kulipa bima ya bidhaa hiyo hadi kufika bandari yako ya karibu. Mfano muuzaji China ameandika USD 300 C&I Dar es Salaam. Basi hapo wewe utauchukua mzigo kiwandani na utahusika na garama zote kuanzia pale hadi unapoupeka isipokuwa muuzaji atakuwa amelipa bima hadi Dar es Salaam.
Pamoja na kuwa zipo Incoterms zingine lakini hizi nilizotaja ndio hutumika mara nyingi. Ukizifahamu hizi utakuwa na mwanga wa kutosha unaposhugulika na biashara kwa njia ya intaneti (ecommerce).

No comments:

Post a Comment

Pages